Sunday, June 13, 2010

WENZETU WAMESONGA MBELE KATIKA KUJIFUNZA KUIMBA.

Wenzetu hawa karibu wapo tayari katika mafunzo yao ya kuimba katika sherehe za kumaliza shule, jana tulikwenda kuiba kwa kuwaangalia wamefikia wapi. Ila hata sisi hatuwaogopi kabisa, tutapambana nao tu! Pia watoto hawa ninao wafundisha wimbo wa kiswahili, wanajivunia sana wimbo huo wa kiswahili; kwakusema sisi tutaimba kwa lugha ya kigeni mpaka watashangaa wao, wamenipa moyo sana. Na sasa tupo kwenye hatua nzuri sana, ila kazi kweli kweli....si mchezo mpaka wajue kuimba vizuri, na mimi nitakuwa sina nywele tena kichwani, kwa kukuna kichwa.

1 comment:

mangi said...

Usichoke kuwafundisha lugha ya Kiswahili kwa kuwa daima watakukumbuka na wewe utakuwa umewachia urithi mzuri sana kwao na vizazi vijavyo.Hongera sana Baraka kwa kuwa mdau mzuri wa Kiswahili huko ughaibuni.Tafadhali sana kaza buti."JARISI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI".

WATEMBELEAJI