Monday, February 21, 2011

JE HUU NI UUNGWANA???

Waathirika wa ajali ya mlipuko wa mabomu ya Gongo la mboto, wakilazimika kujazana kwenye gari kubwa la mizigo, ambalo kwa kawaida hufanya shughuli zake za kusafirisha ng'ombe, mara nyingi huwa ni kuwapeleka machinjioni. Na hii yote ni baada ya makonda wa daladala kupandisha nauli kutoka 250 /= hadi 1000/= na hiyo ni kuanzia Buguruni hadi Gongo la mboto.

Hapo ndipo ninapo uliza; Je huu ni uungwana?
Maana ki binadamu ilitakiwa nauli ipunguzwe na sio kupanda, maana waathirika wa mabomu ni ndugu zetu. Jamani tuwe na uungwana na ubinadamu wa kusaidiana kwenye matatizo makubwa kama haya.

- Kutoka kwa Mkuu Lukwangule.

No comments:

WATEMBELEAJI