Wednesday, February 23, 2011

PETER SCHWINGSHACKL aka. MWALIMU.

Peter, au kwa jina tulilo zoea kumwita.... Mwalimu, akiwa kwenye mtambo wa kujimbia visima enzi zake huko vijijini kwetu Tanzania. Huyu jamaa amefanya kazi nyingi sana hasa za maji katika jamii yetu ya Tanzania. Mimi binafsi namshukuru sana kwa mchango wake mkubwa wa kusaidia jamii, na nimejifunza menge sana kupitia kwake.
Peter akiwa kijiji fulani huko kwetu Tanzania, katika kazi za kusaka maji, na ufungaji wa pampu.

Peter....akifurahi kwa kupigwa picha nyumbani kwake huko mpakani mwa Austria na Italy, katika kijiji cha Welsberg - Monguelfo. Alirudi nyumbani kwao baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu sana kama miaka 16, katika vijiji mbalimbali vya Tanzania katika uchimbaji visima na ufungaji pampu, hasa za kutumia upepo (windmill). Nimejifunza mengi sana kwa kufanya nae kazi.
-Asante sana Peter kwa mchango wako wa hali na mali...katika huduma ya maji vijijini Tanzania.


No comments:

WATEMBELEAJI