Sunday, February 27, 2011

TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI!

TUKIMWEKA MUNGU MBELE YA KILA KITU; TWAYAWEZA MAMBO YOTE!


Twayaweza mambo yote katika yeye atutiae nguvu, yote yanawezekana katika jina la Mwenyezi Mungu.
Nia zetu zamfurahiya Bwana, soma maneno mazuri na matamu kama haya; Hatuta mwacha Mungu hata watutenge, hatuta ogopa hata wakitucheka, haturudi nyuma hata watudharau, hatubabaiki hata kidogo.....watake wasitake.

Fadhili zake ni nyingi tena ni mpya kila siku, tena yeye hapendelei....atenda haki kwa kila mmoja. Ana bariki, ana fariji, ana okoa, ana samehe.
Mungu ndiye Baba yetu na Bwana mkuu wa wakuu.

- JUMAPILI NJEMA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU.

No comments:

WATEMBELEAJI