Sunday, February 20, 2011

UKOMBOZI WETU WATOKA KWA MUNGU WETU!

Ukombozi wetu watoka kwa Mungu wetu... aketie juu ya kiti cha enzi, na kutoka kwa mwana kondoo. Bwana unilinde nami sikuachi daima Bwana wangu, Bwana uniokoe kwa huruma yako nisikilize nakukimbilia Bwana wangu wewe pekee ni ngome yangu na mwamba wangu.

Ee Bwana nifanye mimi niwe huru, kwani mimi ni mtumwa wa tamaa zangu...uniongoze kuwa mwaminifu daima. Bwana niokoe katika waovu, walio nitega ili nianguke, wewe pekee ni mkombozi wangu, utaniokoa! Ninakukabidhi roho yangu kwani wewe pekee u mwaminifu katika maisha yangu, kwani mimi nimelegea mwili na roho vipo taabani. Na maisha yangu ni tabu tupu, miaka imepita naendelea kuwa na dhiki, maisha yangu ni dhiki tupu.
Maadui zangu wananicheka mimi, marafiki zangu na wana jamaa na kila mtu anionae ananiepuka. Wewe pekee Bwana Mungu wangu unaweza kunisaidia.

-TUMWOMBE MUNGU KATIKA MATATIZO YETU MBALIMBALI, NAYE ATAYATATUA TU! TUWE NA IMANI ZAIDI NA YEYE BABA MUNGU MKUU.

1 comment:

Anonymous said...

I love this and my life will very normal according to this

WATEMBELEAJI