Friday, March 4, 2011

HALI HII INASIKITISHA SANA......KUTOKA KWA DADA SUBI HII.

Nilikutana nayo habari hii kwa Dada Subi wa WAVUTI. Hapo kijiwe cha Facebook.

Hilo ndilo gari la zimamoto la uwanja wa ndege wa Nduli - Iringa, 2011. Sisi Watanzania tuna dharau sana na kuchukulia mambo ''simpo'' na kuwa kiherehere wa kujitetea ''ndiyo uwezo wetu'' wakati Oysterbay, Mbezi, Masaki nk, havifanani kabisa na zimamoto hili....aka booom...!!!! eh eh! Mungu epushia mbali.

- Kweli kabisa Dada Subi usemi wako nakubaliana nao, vitu vingine huwa tunavifanyia mchezo kabisa, hivi kweli li ndege hilo likiwaka moto hapo hicho kijamaa kinaweza kuzima moto kweli? ama kweli Bongo ni tambarare kwa kila kitu. Hicho kijamaa hakiwezi kuzima hata jiko la mkaa likiwaka moto, halafu kizime ndege kubwa namna hiyo, hivi tuna utani na roho za watu kweli! Isitoshe hapo usije kukuta hakina hata maji, kweli kabisa sijui tufanye nini Tanzania ili tusichezee na kuleta mchezo wa maisha ya watu na riho za watu. Kila siku ufahari wa mashangingi tu, maisha je? Vitu muhimu je?

No comments:

WATEMBELEAJI