Friday, March 4, 2011

IDADI YA MBUMBUMBU YAZIDI KUONGEZEKA TANZANIA.

ELIMU YA WATU WAZIMA;


Idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika hapa nchini, inaongezeka kwa wastani wa asilimia mbili kila mwaka. Hali hii inayoiweka Tanzania katika wakati mgumu wa kutimiza malengo ya mkataba wa Elimu kwa wote (EFA).
Mkataba huo unataka idadi ya watu wa kundi hilo ipungue hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2015. Haya yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamis Dihenga, katika hotuba yake ya uzinduzi wa stashahada ya Elimu ya watu wazima itakayokuwa ikitolewa kwa njia ya masafa. Hata hivyo hotuba ya Katibu Mkuu ilisomwa na Mkurungenzi wa Elimu ya watu wazima katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Salum Mnjagila.
Profesa Dihenga, alisema; kuanzishwa kwa stashahada hiyo kutatoa fursa kwa watu wazima kujifunza kusoma na kuandika. Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya watu wazima, Lamberpha Mahai, alisema; lengo la mpango huo ni kuwa watu wenye elimu ya kutosha, ambao watasaidia kutoa mafunzo kwa watu wazima wasiojua kusoma na kuandika.

No comments:

WATEMBELEAJI