Tuesday, March 29, 2011

KABURI LA BABA MTAKATIFU PAPA YOHANE PAULO II.

Hapa ndipo alipozikwa Papa Yohane Paulo II, nilienda kutembea mwaka 2006...makaburi ya mapapa wote yapo chini ya Kanisa la Mt.Petro, Vatian City. Nilipata msisimko sana baada ya kufika kaburini hapo, maana nilikuwa nampenda sana huyu Papa. Yeye alipenda sana azikwe chini ya ardhi na kaburi la kawaida kabisa, jinsi alivyoomba yeye kwa maandishi yake wakati wa uhai wake, tofauti na makaburi ya mapapa wengine ambao makaburi yao makubwa yaliyojengwa kwa umalidadi, angalia hapa picha za chini;


Makaburi ya Mapapa wengine....huko chini kuna makaburi mengi sana, mapapa wote wamezikwa hapa.

No comments:

WATEMBELEAJI