Tuesday, March 29, 2011

MAANDALIZI YA SIKU YA VIJANA KIMATAIFA YAZIDI KUCHARUKA!

HABARI KUTOKA VATICAN CITY KWAAJILI YA SIKU YA VIJANA DUNIANI, 2011. ITAKAYOFANYIKA HUKO MADRID - HISPANIA, INASEMA; Mpendwa sana kijana, maandalizi kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani kwa mwaka 2011, yanazidi kupamba moto huko Nchini Hispania - Madrid. Makala yetu sambamba na kuwaalika kujikita katika maandalizi ya maadhimisho hayo, kwa namna ya pekee; kuhusiana na mikakati mbalimbali inayoendelea kilele cha maadhimisho hayo. Habari zilizotufikia hivi karibuni ni pamoja na taratibu za kuwa na hija maalumu katika majimbo yote 63 ya Kikatoliki nchini Hispania, tukio linalotarajiwa kufanyika kati ya tarehe 11 hadi 15 mwezi wa Agosti, 2011. Taratibu zinaendelea kufanyika ili kuwawezesha vijana wote takribani 300,000 toka pande mbalimbali Duniani, kutembelea maeneo mbalimbali ya majimbo nchini humo kama sehemu ya hija ya siku ya vijana Duniani. Kulingana na msemaji na mratibu wa shughuli hizi za siku ya vijana Kimataifa nchini Hispania, Javier Igea, hija hizi zinatarajiwa kugharimiwa na majimbo hayo, ikiwemo kuihusisha Jamii ya waamini kuhakikisha kuwa washiriki wanapatiwa malazi bure. Shughuli zitakazofanyika wakati wa hija hizi za kimajimbo ni pamoja na shughuli za kitamaduni, kutembelea maeneo ya kihistoria na kumbukumbu mbalimbali. Kitakuwa pia ni kipindi cha kusali na kutembelea madhabahu mbalimbali yanayopatikana katika majimbo hayo kwaajili ya kusali. Hadi tunapata taarifa hizi zaidi ya vijana 300, 000 wamekwisha jisajiri kwa ajili ya kushiriki matukio mbalimbali ya siku hiyo ya vijana, kuanzia tarehe 16 hadi 21 Agosti, 2011. Wakati idadi kamili inatarajiwa kufikia vijana Millioni moja nukta tano. Siku ya vijana iliyofanyika nchini Australia kunako mwaka 2008, vijana laki tatu na nusu kutoka katika nchi mia moja na sabini walihudhuria katika maadhimisho hayo, katika kilele chake wakati wa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita. Wakati huo huo baadhi ya majimbo nchini Hispania yamejitolea kugharimia gharama zote za kushiriki kwa vijana wanaotoka katika mazingira magumu kama vile; Haiti ambapo hadi sasa jumla ya vijana 260 watafaidika na program hiyo, vijana 250 watagharimiwa kutoka nchini Puerto Rica. Sambamba na ufadhiri huo, kumeandaliwa pia shindano kwa ajili ya waandishi wa habari juu ya mada walinzi wa wakati ujao ''Watchmen of the Future'', kaulimbiu iliyopendelewa sana na Mtumishi wa Mungu, Papa Yohane Paulo II...katika kuwatambulisha vijana. Shindano hili litakuwa na zawadi maalumu ambayo itatolewa kwa kazi zote zitakazochapwa kabla ya mei mosi mwaka huu zikionesha maana ya siku ya vijana Duniani huko Madrid. Tukiendelea kuwaalika kila mmoja wenu kutafakari umuhimu wa tukio hili katika ulimwengu wetu wa vijana mamboleo. -Ni siku nzuri sana upatapo nafasi, usisite kwenda Madrid - Hispania.

No comments:

WATEMBELEAJI