Monday, March 28, 2011

NCHINI VATICAN.....NCHI ILIYOPO NDANI YA NCHI NYINGINE!

Nchini Italy kuna pia nchi ndogo mbili ndani yake ikiwemo; Vatican na S.Marino. Ni nchi ndogo sana kama vile Mkoa tu....lakini ni nchi ambazo zinajitegemea. Mara nyingi mimi huenda Vatican pindi nipatapo nafasi ya kwenda Roma ki kazi au kutembea, Napenda sana Vatican jinsi ilivyo pia ni makao makuu ya dini ya Kikatoliki Duniani, na mimi kama Mkatoliki. Lakini hizi picha nilipiga mwaka 2006 wakati nilipoenda kutembelea kaburi la Papa Yohane Paulo II, Papa huyu nilikuwa nampenda sana, kutokana jinsi alivyo badilisha ulimwengu huu kwa mambo mengi mazuri...hasa ulimwengu wa vijana. Nilipata bahati ya kwenda kutembelea kaburi lake, ilikuwa ni furaha sana kwangu. Picha hazionekani vizuri, lakini ni kumbukumbu pekee niliyo nayo, na kesho nitaweka picha ya kaburi lake kabisa, bado najaribu kutengeneza maana nilipiga haraka haraka tu kutokana na foleni kubwa iliyokuwepo kutembelea kaburi hilo. Haikutoka vizuri, lakini nitajitahidi kuitengeneza walau kuirekebisha kidogo.
UWANJA WA VATICAN, MBELE YA KANISA KUU LA MT.PETRO.
NDANI YA KANISA LA MT.PETRO, MJINI VATICAN.
KATIKATI YA UWANJA WA VATICAN.

1 comment:

Mama Pam Augusta said...

ni nchi niipendayo sana natamani sana siku moja nihudhurie ibada ambayo papa anasoma misa ila ndo sijui lini, siku ipo kwani hazigandi.

WATEMBELEAJI