Thursday, March 24, 2011

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA DADA YASINTA KWA KUFIWA.....

.....NA MDOGO WAKE MPENDWA SANA ASIFIWE.

PICHA NI MAREHEMU ASIFIWE ENZI ZA UHAI WAKE.
MAREHEMU ASIFIWE NGONYANI 26/11/1989 - 23/03/2011.

MANENO YA DADA YASINTA KATIKA BLOG YAKE YA MAISHA NA MAFANIKIO;

Jioni hii muda si mrefu nimepigiwa simu kuwa sina mdogo tena. Mdogo wangu mpendwa na wapekee ametuacha amekata roho jioni hii kama saa tatu kasorobo ya TZ. Mwenyezi Mungu na aipokee roho yake mahali pema peponi, Amina.
HAKIKA NI PIGO KUBWA SANA KWA FAMILIA YETU.
- Yasinta Ngonyani.




Dada Yasinta ni mdau mkubwa sana wa Blog hii, hutembelea na kutoa maoni yake mara kwa mara. Nasi tunatuma salamu zetu za rambirambi na kumpa pole sana kwa kufiwa na mdogo wake mpendwa sana Asifiwe, nasi tupo pamoja nawe Dada Yasinta katika msiba huu mzito, kwa maombi na sala zetu kwa Mwenyezi Mungu. Poleni sana ndugu na jamaa wote mliofiwa, Mwenyezi Mungu awapeni nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Asifiwe, Amina!
BWANA AMETOA, NA TENA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIBARIKIWE! AMINA.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Baraka Ahsante sana kwa ushirikianao wako. upendo daima!!!

WATEMBELEAJI