Thursday, March 3, 2011

USHAURI KWA VIJANA WENZANGU.....USICHAGUE KAZI!

Mara nyingi imetokea kwa vijana wenzangu wengi kuchagua kazi, kwa sababu mbalimbali; oh mimi nimesoma sana si stahili kufanya kazi hiyo, oh mimi hivi...oh mimi pale! Sasa kama huwezi kupata kazi uliyosomea ndo ikufanye ulale na njaa??

Kwa ushauri wangu zaidi; kama huna uwezekano wa kupata kazi uipendayo au uliyosomea, basi fanya kazi yoyote ile uipatayo muda huo bila kuchagua, ukisubiri kupata kazi uipendayo na uliyosomea. Kijana mzima uliye na nguvu zote huwezi kukaa tuu bila kutofanya kazi, kwasababu unasema; mimi kazi hii siipendi, sijasomea, oh sijazoea..nk. Sababu kedekede.

- Maisha bila kujishughulisha hayaendi kabisa...kijana mwenzangu. Piga mzigo mafanikio utayaona mwenyewe!

No comments:

WATEMBELEAJI