...MAANA HII MIAJALI KILA SIKU HAPO MORO KUNA NINI JAMANI? ahhhh....!!!!! Baadhi ya majeruhi waliolazwa wodi namba tatu, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Majeruhi 17 walilazwa katika Hospitali hiyo baada ya Daladala walilokuwa wakisafiria kutoka Mikese kwenda Morogoro mjini, kugongana uso kwa uso na Lori la mizigo. Watu sita wamepoteza maisha yao kutokana na ajali hiyo iliyotokea alfajiri leo Aprili, 5. 2011. Katika eneo la Mkambarani barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam. - Picha na John Nditi - Morogoro.
No comments:
Post a Comment