Habari zenu wadau wangu na wapendwa wangu, nimewasili tena hapa kuwa nanyi kwa mara nyingine tena, baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kidogo nikiwa likizo huko nyumbani Tanzania. Salamu sana kutoka nyumbani. Likizo yangu imeenda vizuri sana na kuwa na mafanikio mengi. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kuniwezesha kwa yote kwa ujumla. Hasa kwa kusafiri salama safari zangu zote, za Tanzania na mpaka kurudi salama hapa Italy.
Asanteni sana pia nyinyi wadau wangu kwa sala zenu, na poleni sana kwa usumbufu wangu wa ukimya wangu. Kwasasa nasema tupo pamoja tena kwa mara nyingine.
Nawasalimu sana tena sana na kuwakaribisha tena tuwe pamoja kama kawaida katika kijiwe hiki cha KAZI YAKO NI JINA LAKO.
Ni mimi wenu wa siku zote Baraka wa Chibiriti.
2 comments:
ha ha ha haaaaa! Mweeh, Una bahati wewe yaani hapa nilikuwa napiga mahesebu ni vipi na ni polisi ipi ni rahisi kuripoti kuwa tumepotelewa na mtu...Karibu sana sana kaka Baraka..najua una mengi ya kusimulia. Kwa kweli tume/NIMEKUMISS sana. Karibu ...
ha ha ha haaaaaa.....Dada Yasintaaaa, kumbe ndo hivyo polisi tena. Nafurahi kuwa mnanijali mpaka mwende kuripoti?
Asante sana tena sana Dada Yasinta, hata mimi nilikuwa nimekumiss/kuwamiss sana tena sana.
Post a Comment