Wewe Bwana usiniache, Mungu wangu.....usijitenge nami, ufanye haraka kunisaidia...ee Bwana wokovu wangu.
Ee Mungu Mwenyezi na mwenye huruma, wawajalia waamini wako neema ya kukutumikia vema na kwa uchaji. Tunaomba utuwezeshe kukimbilia ahadi zako pasipo kukwaa.
Ee Bwana tunaomba neema yako izidi kutenda kazi ndani yetu, na tena ituweke tayari kupokea ahadi za sakramenti hizi zilizotuburudisha.
No comments:
Post a Comment