Sunday, November 6, 2011

TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI HII.

Ee Mwana wa Mungu, unifanye leo nishiriki kwenye karama yako.....karama ya kiroho. Sita ifunua siri kwa maadui zako, wala mimi sita kupa busu kama lile la Yuda....bali kama yule mwizi uliyeteswa naye pembeni mwa msalaba. Ninakuomba ee Bwana unikumbuke mimi katika ufalme wako. Ninakuabudu Bwana kifudifudi....ni siri kubwa ee Mungu uliye hai, uliye kweli chini ya maumbo haya ya mkate na divai, mimi ninajinyenyekesha sana mbele yako, karibu Bwana njoo kwangu ukae nami. Huu ni mwili na damu kweli ni hakika nikiona mbingu zote na nikionja ni Yesu mwenyewe....mimi hali hii nasadiki, aliyejitoa kwaajili ya ulimwengu, fumbo hili ni la kweli imani yangu inaelewa kabisa hili. Jirani naomba pokea kwangu nyoyo takatifu, ninarudishiwa nguvu mpya bila shaka....Ekaristi huimarisha upendo moyoni, yarudisha imani, furaha iliyopotea....karama hii ni kinga na dawa safi ya moyo wangu....dawa safi ya roho!

No comments:

WATEMBELEAJI