Katika kujenga na kuimarisha Jamii yoyote ile.....upendo unapaswa kupewa nafasi ya kwanza kabisa, kwamba; tunaweza kufanya yote lakini kama hatuna upendo sisi ni kama sauti ya debe tupu. Kumbe ni kwa njia ya chemchemi ya ndani ya upendo ambapo tunu za kweli, uhuru na haki zinajengeka, kukua na kukomaa. Maisha ya binadamu yamepangwa na kuzaa matunda yenye manufaa na kuendana na heshima ya binadamu inayopatikana katika ukweli iwapo maisha yatakuwa na haki, yaani; haki zinazoonekana kuheshimika na kwa uaminifu kutekeleza shughuli zinazoendana, zikisaidiwa na roho ya kutokuwa na ubinafsi ambao unafanya mahitaji ya wengine yanaonekana kama ya mtu mwenyewe na kuongeza umoja wa mambo ya thamani ya kiroho na kujali mahitaji ya muhimu. Yanapokamilishwa katika uhuru wenye kunufaisha wote, wanaamshwa na akili ya asili inayokubaliana na wajibu katika matendo. Tunu hizi ni nguzo zinazotoa nguvu, na moja kwa moja kuimarisha nia au maisha na matendo. Hizi tunu zinapima ubora wa maisha ya Kijamii.
Upendo hutanguliwa na upo juu ya haki, ambao ni lazima upate ukamilifu wake katika matendo ya huruma. Iwapo haki yenyewe inafaa katika kuamua kati ya watu wanaohusika katika kutoa na kupokea ugawaji wa mali katika hali ya usawa, upendo....na ni upendo tu una uwezo wa kumfanya binadamu awe mwenyewe. Mahusiano ya binadamu yanatawaliwa tu kwa kipimo cha haki.
Mang'amuzi yaliyopita na kwa njia za nyakati zetu peke yake hazitoshi, zinaweza kurudisha nyuma na kuuharibu ukweli huu. Kila eneo la mahusiano katika haki lazima isahihishwe kwa kufikiria kiwango cha upendo ambao una tabia ya huruma ya mapendo. Hakuna sheria ya mfumo wa taratibu au upatanisho utakaoweza kufaulu kweli kwa kushawishi watu na nchi, kuishi maisha ya umoja, undugu na amani....hakuna namna ya kufikiri itakayozidi jitihada za kutafuta upendo. Ni upendo katika thamani yake kama aina ya fadhili, unaoweza kuongeza na kuweka sura ya maingiliano ya Jamii kuelekea kwenye amani katika mazingira ya dunia inayoendelea kuwa ya mchanganyiko. Ili yote haya yawepo, hata hivyo umakini unaweza kuchukuliwa kuonesha upendo na sio tu jukumu la kuamsha matendo ya binafsi, bali nguvu yenye uwezo wa kuchochea njia mpya za kukabili matatizo ya dunia ya leo, katika kufanya upya miundo ya msingi, muundo wa Jamii, mfumo wa sheria kutoka ndani ya mfumo wenyewe.
Kwa mtazamo huu, upendo unachukua tabia ya mtindo wa huruma Kijamii na ya Kisiasa. Huruma ya Kijamii inafanya tupende manufaa kwa wote inatuwezesha kikamilifu kutafuta manufaa kwaajili ya watu wote, na siyo kama mtu binafsi bali pia vipengele vya Jamii vinavyowaunganisha.
Jamii na huruma ya kisiasa haimalizii katika mahusiano ya watu, lakini inaingia katika mtandao unaojengwa na uhusiano huu, ambapo ni Jamii ya Kijamii na ya kisiasa, inayoingilia katika mahitaji ya manufaa kwa wote. Katika mambo mengi jirani anayepaswa kuonyeshwa upendo anaishi ndani ya Jamii, hivyo kumpenda kiuhalisi, kumsaidia katika mahitaji yake au katika umaskini wake inaweza kumaanisha kitu zaidi ya mahusiano tu kati ya watu.
Kumpenda Kijamii inamaanisha kuangalia mazingira, kutumia njia za mifumo ya kijamii ili kuboresha maisha yake na kuondoa vyanzo vya Kijamii vinavyoleta umaskini. Bila shaka tendo la upendo, kazi ya huruma na kwa njia hizo mtu hujibu hapa na sasa mahitaji ya jirani, lakini pia ni lazima tendo la upendo liwe katika kujipanga kwa Jamii na kuweka muundo, unaomwezesha jirani kutobaki kuishi katika umaskini. Hasa kama hali hii inakuwa ya watu wengi na nchi ama sehemu ya kundi la watu, hapo linakuwa suala la Kijamii ambalo litaangalia katika upana wake.
Ndio maana mimi husema daima kwamba; dunia ya leo haina njaa ya chakula na mahitaji mengine ya binadamu ila ina njaa ya upendo, bila shaka na njaa ya kutojali manufaa kwa wote, huu ndio ukweli tukiangalia utajiri huo basi kusingekuwa na sababu ya baadhi ya watu kuwa na mateso.
No comments:
Post a Comment