Monday, January 23, 2012

CHAMA 1 NCHINI ITALY...CHA TUDHALILISHA WATANZANIA!

Chama cha KiSiasa nchini Italy, maarufu kama LEGA....kimetudhalilisha sana Watanzania..... Kwa hela zilitolewa na Serikali ya Italy kwa ajili ya kuinvest Tanzania, kwaajili ya mambo fulani huko kwetu....sasa wafuasi wa Chama hiki Cha Lega wamekuja juu kwa maandamano tena kwa Bendera yetu ya Taifa, wakisema; Watanzania tunaomba hela zetu mrudishe, yaani ni katika kutudhalilisha kama Taifa; tena hata picha hiyo ya bendera yetu wameweka maneno ya kutukashifu tu! na nembo yao ya Chama chao hicho kwa pembeni.....sasa sisi wapi na wapi tunaitwa; PANZANIA?

Mimi naamini Ubalozi wetu nchini Italy utalichukulia hatua swala hili, kuwafikishia wahusika ili walifanyie kazi swala hili......na naomba sana msilifumbie macho.

- HAYA SASA MAMBO HAYA; WATANZANIA TUNAOMBWA TURUDISHE HELA ZA WATU, JE IMEKAEJE HII JAMANI????

2 comments:

lukwangule said...

Mzee chibiriti hii inakuaje vile mbona sijaielewa fedha za nini walizoleta? Chama au serikali si waisute serikali yao ama

Baraka Chibiriti said...

Hapo wanataka warudishiwe pesa zao, zilizotolewa huko kwetu Tz

WATEMBELEAJI