Thursday, January 19, 2012

SAHANI YANGU YA UJAMAA IMEANDIKWA....TANZANIA!



Nyimbo hizi zinanikumbusha mbali sana, enzi hizo za utoto wangu huko Ugogoni....ilikuwa napenda sana kuimba na kuzicheza, ungefanikiwa kuniona jinsi nilivyokuwa hodari wa kuchezesha mabega na kuzungusha kichwa mpaka ungefurahi mwenyewe, ilikuwa inaruhusiwa kwa watoto na wanawake...kucheza kwa kuzungusha kichwa na mabega, kwa wanaume marufuku, kwa Wanaume ni kucheza kwa kikakamavu na kukanyaga chini kwa nguvu zote huku umevaa vikengele fulani miguuni vinavyotoa sauti nzuri a.k.a (CHINDA) . Tukiwa na wenzangu tunashindana kucheza ilikuwa raha sana, natamani sana kurudi utotoni...lakini basi hamna jinsi.
Sisi huu wimbo tulikuwa tukiuimba hivi; Sahani yangu ya Ujamaa imeandikwa Usife moyo! Maana tulikuwa na Lori la Kijiji chetu lilikuwa limeandikwa; USIFE MOYO, na maneno mengine lilikuwa limeandikwa; NKIGAILA NENE NDAGWA = Nitajitegemea mimi mwenyewe Sungura....walikuwa wanamaanisha kujitegemea wenyewe kama Kijiji, bila kutegemea Serikali. Na kweli Kijiji kilijitegemea kwa mambo mengi sana.


- ASILI YANGU SIWEZI KUISAHAU HATA KIDOGO!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ukiisahau ASILI YAKO UTAKUWA NA DHIDA MAALUMU. Safi sana kaka Baraka nimeupenda huu wimbo ..sahani yangu... haupo peke yako ambaye unatamani kuwa mtoto tena ..ila basi sasa:-(

Baraka Chibiriti said...

Asante Dada Yasinta......

WATEMBELEAJI