VUMBI; Ugumu wa kazi hii ya uchimbaji visima vya maji, wakati mwingine huwa ni mwendo wa vumbi tu, mita hadi mita....nakumbuka kisima hiki mpaka mita 70 ilikuwa ni vumbi tu, Peter alitukana matusi yote akamaliza; ya Kijerumani, Kiitaliano na Kiswahili mpaka Kigogo, maana wapimaji walisema Mita 60 kuna maji.....tukaenda mpaka 90 ndipo tukakutana na maji. Wapimaji hao ni Wafanyakazi wa Idara ya Maji Serikalini. Kazi hii ilikuwa ni; Jua, Tope, Vumbi, usiku Mbu, na Mahangaiko mengine mengi.....lakini naipenda mpaka sasa, maana watu wa Vijijini walikuwa wakifurahi sana wakiona tumepata maji...nilipoona watu wakifurahi nilikuwa najisikia vizuri sana.
TOPE; Peter Schwingshackl, a.k.a Chuma Kigumu cha zamani (Hakipati kutu, hata kikipata hakichakai)....au tulikuwa tukimwita Mwalimu, akiwa katika mtambo wa kuchimbia visima katika Kijiji cha Hongoro - Mkoka, Dodoma.
TOPE; Kazi ikiendelea.
MAJI; Hapa ni furaha kweli kuona kazi imefanyika na maji mwaaaa......Peter akiwa na watoto mbele ya kisima kimpya.
MAJI; Furaha yake ndio hii....ukiona maji yanatoka kwa wingi, hasa eneo lenye shida sana ya maji. Kumbukumbu yangu hii na tamaa yangu ya kurudi tena katika mambo haya.
No comments:
Post a Comment