Friday, January 20, 2012

ENZI HIZO ZA UCHIMBAJI VISIMA HUKO VIJIJINI AU PORINI.

Aliyekuwa Boss wangu Peter Schwingshackl, hakuwa nyuma katika kazi za kusaka Maji Vijijini....huko Vijijini ilikuwa hakuna kuchagua nini cha kula, kama ni legelege unakula jeuri yako. Peter alikuwa akisema daima; Kazi za porini kama sio chuma kigumu huwezi, yeye alikuwa akijiita Chuma cha zamani hakizeeki...hata kipate kutu. Kweli jamaa huyu Peter alikuwa chuma kigumu, tulihangaika naye usiku na mchana katika shida mbalimbali za porini.
Mzee Bakari, moja ya Wazee ambao wamenifundisha kazi ni nini na maisha ni nini....akipata kitoeo chake hapa, huko Kijijini kwenye kuchimba Kisima. Bado nakumbuka wema wa Wanavijiji wengi, waliokuwa wakituletea chakula. Kwakweli kazi hii ni nzito sana na ngumu sana, lakini naikumbuka sana na kutamani sana kurudi tena.

No comments:

WATEMBELEAJI