Wednesday, January 25, 2012

ZAWADI YA MJENGWA KWA WANA VIJIJI WALIO WENGI.

ZAWADI YA MKUU MJENGWA YA GAZETI LA KWANZA JAMII, nimeipenda sana hii;

Maneno ya Mjengwa akisema hivi; Kwenye safari zangu natembea na akiba ya Magazeti. Njiani nikisimama kunyoosha miguu hupenda kuwaachia wenyeji zawadi ya Gazeti. Huko Vijijini tunakopita, kuna wengine imepita miaka hawajakamata gazeti.

- Hata mimi nakumbuka sana nilipokuwa nasafiri sana Vijijini miaka ya nyuma, watu wengi walikuwa wakiomba magazeti, ukiwapa hata yaliyopita zaidi ya miezi 2 wakati mwingine hata zaidi ya miezi 2...wanafurahi sana kusoma kupata habari hata zilizopita. Nakumbuka ilikuwa ni furaha sana tena sana kwao kupata gazeti na hasa vijana walikuwa wakiomba sana Magazeti ya michezo, tena mara nyingi nilikuwa nikishuhudia wanaanza kubishana kwa kusema; si unaona nilikuwa nawambieni mchezaji fulani yupo hivi na vile, nyinyi mlikuwa mnabisha....sasa si mnaona hata gazeti limeandika kabisa, nilikuwa nacheka sana maana habari zenyewe zilikuwa za siku nyingi zimepitwa na wakati, nakumbuka sana story kama hizi zilikuwepo mara kwa mara ukiwapa magazeti. Nimeona picha hii kwa Mjengwa, nimekumbuka mbali sana, na kutamani sana kurudia tena kazi yangu ya Vijijini.

No comments:

WATEMBELEAJI