Wednesday, February 29, 2012

MAMBO YA KUZIBA PANCHA....ILULA - IRINGA. 2011.


Tulipata pancha, tukitokea Makalala - Mafinga - Iringa....sehemu ya Ilula, baadae tulipata sehemu ya kuziba tairi kabla ya kuendelea na safari yetu ya kurudi Dar es salaam. Nilipata pia nafasi ya kuongea (kupiga story kidogo) na hawa vijana wa Kijiwe hiki cha kuziba pancha cha Ilula, wanachekesha sana tena sana....nilicheka mno, na kusahau kabisa shida na matatizo niliyonayo, mara nyingi huwa tunajisahau sana ukipata shida kidogo tu, unalalamika weeee...!!! hujui kumbe kuna wenye shida zaidi yako. Vijana hawa pamoja na kuwa na uchumi wao mdogo, lakini hapa ni full shangwe haswa. Nilijiona kwakweli mimi ni mlalamikaji tu, hakuna cha shida wala tabu. Walinichekesha mpaka leo nakumbuka kwa hili, Walisema; Hapa huwa wanakuja wenyewe Viongozi wakubwa na vitambi vyao kuomba tuwazibie pacha, huwa wakati mwingine wanakuja kwa kuamrisha ziba haraka nina safari ndefu, na sisi tukiona hivyo ndo kwanza tunalegeza uzi, utaona wenyewe wanaanza kuomba kwa utaratibu - wananywea wenyewe! Kazi ya mtu ni kazi tu...lazima uiheshimu bwana, kwani mimi sio binadamu kama yeye? hata awe nani akifika hapa lazima atulize mpira tu! Sisi hatumwibii mtu, tunafanyakazi na kujali watu wanaotujali...ukileta ubishi wako na sisi tunakuwa hivyo hivyo, walisema vijana hawa.

Nilicheka sana na kufurahi mno kwa msimamo wa hawa vijana....kweli inatakiwa iwe hivi; heshimu kazi ya mwenzio, hata uwe mkubwa kiasi gani...heshimu wadogo tafadhali.

No comments:

WATEMBELEAJI