Friday, March 16, 2012

MAMBO HAYA NI AIBU SANA KWA TAIFA LETU JUU YA MICHEZO!



Leo nilikuwa naangalia Taarifa ya Habari kwenye TV moja ya Taifa la hapa Italy.......nikakutana na habari hii; ya fujo zilizotokea katika Uwanja wa Taifa Dar es salaam, mechi kati ya Yanga na Azam. Nimesikitika sana tena sana na kuona aibu mno, tena ukichukulia mimi ni mshabiki wa Timu ya Yanga damu.....sikutegemea kabisa mambo kama haya yangefanyika na wachezaji wa Timu kubwa nchini kwetu kama ya Yanga. Alinipigia simu mara moja rafiki yangu Mwitaliano, akaniambia; angalia kwenye TV wanaonyesha habari kuhusu Timu ya Yanga ya Tanzania, bahati nzuri nilikuwa hapa nyumbani kuangalia nakutana na hii, ingawa nilishakuwa tayari na taarifa hizi mbaya, sikutegemea kama Taarifa hii ingeonyeshwa mpaka huku Ughaibuni. Aibu sana kwa sisi Wanamichezo wa Tanzania.

No comments:

WATEMBELEAJI