Monday, March 5, 2012

RAFIKI SIMON MGOGO....KATIKA KUCHORA PICHA ZA KIBONGO!

Simon Mgogo a.k.a Mwalimu (Maestro) wamemkubali kwa kuchora michoro mizuri ya Kiafrika huko Mkoa wa Umbria - Italia. Mpaka kufikia kumtoa katika Gazeti la Mkoa huo. Mgogo anaishi huko Mji wa Perugia katika Mkoa huo wa Umbria, yupo kwa muda mrefu sasa huku Italy, alikuja kwaajili ya kuendeleza kipaji chake cha uchoraji na kuamua kubaki huku huku baada ya kumaliza masomo yake.....baada ya kuhangaika huku na kule katika kazi mbalimbali za maisha ya hapa Italy, hatimaye wamemkubali na kuingia katika mfumo wa uchoraji Kitaifa. Mara nyingi sana nilienda kumtembelea huko Perugia, pia yeye alikuja mara nyingi hapa Cesena kunitembelea, maana tulikuwa tunafahamiana kutoka Tanzania, na nilikuwa nafahamu kuhusu kipaji chake cha uchoraji na mara nyingi sana nilimshauri kwanini asirudie kazi yake ya uchoraji maana mimi nilikuwa napenda sana michoro yake aliyochora huko Tz, yeye alikataa kata kata kurudia kazi hiyo bila kutoa sababu yoyote, nilisikitika sana kwa kujua kipaji chake...lakini yeye hakujali kabisa. Mpaka hapo alipompata rafiki wa kike Mwiitaly (Chiara) Hapo ndipo alipomshauri na kukubali kurudia kazi hii, na matunda ni haya! Kwakweli sisi wanaume ni dhaifu daima kwa akina mama, tupende tusipende! Mimi nilimshauri alikataa kata kata, lakini Chiara mara moja....kazi kweli kweli...!!!!!!
Simon Mgogo kabla hajaja huku Italy, alikuwa pia ni mchora Katuni katika Gazeti moja maarufu Tanzania miaka ya nyuma, alijulikana sana na katuni yake ya MZEE MANJE.

Nimemtumia hongera zangu nyingi....na tena namtumia hapa, maana na yeye pia ni mfuatiliaji wa blog hii; HONGERA SANA MWALIMU SIMON MGOGO a.k.a MZEE MANJE.



Baadhi ya picha alizochora Simon Mgogo.
Nikiwa na Simon Mgogo, nyumbani kwake Perugia.
Pamoja na Simon Mgogo na Mchumba wake....huko Perugia - Umbria, Italy.

1 comment:

WATEMBELEAJI