KICHEKESHO CHA LEO!
Kuna Mmasai mmoja alikuwa na tabia kila anachonunua lazima ajaribu kwanza ndipo atoe pesa, siku moja alikwenda kwenye duka la mpemba mmoja pale Pemba kununua kiberiti akaagiza, kama kawaida yake alianza kujaribisha njiti kama zinawaka... akajaribu ya kwanza ikazima, ya pili ya 3 mpaka zote zikawa zinazima kwaajili ya upepo. Mwisho akasema nipe kiberiti kingine hiki hakiwaki... Mpemba kupokea kiberiti hakina kitu, kuuliza njiti zipo wapi? Mmasai akajibu nimejaribu zote haziwaki!! Weeeeeee kilichoendelea hapo mi sikuwepo!!!! Ha ha haa...!!!!!
No comments:
Post a Comment