Saturday, March 27, 2010

AJALI YA KIBAMBA- DAR ES SALAAM WATANO WATAMBULIWA.







Maiti tano kati ya 11 wametambuliwa waliokufa eneo la kibamba darajani - Dar es salaam, katika ajali iliyohusisha lori la mafuta na daladala. Ajali hiyo iliyoiacha daladala lenye namba za usajili T 615 AJW likiwa kama chapati baada ya kuangukiwa na lori hilo lililobeba mafuta ya taa, lori hilo aina ya IVECO FIAT lenye namba za usajili T189 ABP na Trela lake T192 ABP, lori hilo lilikuwa likielekea Isaka - Shinyanga.
Taarifa za mashuhuda zinasema kwamba abiria wote waliokuwa ndani ya daladala hilo walikufa huku wengine wakibaki vipande na viungo vikitengana na miili.
Lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Kudra Adam (30) ambaye alikimbia baada ya ajali, ambapo lori hilo linamilikiwa na Mohamed Mahmoud, huku mmiliki wa daladala hilo akijulikana kama Seleman Khalfan Rajabu.
Ajali hiyo iliwakusanya mamia ya wakazi wa Kibaha kwaajili ya kuwatambua ndugu zao. Miongoni mwa waliotambuliwa ni; Shukuru Hussen (27) aliyetambuliwa na Baba yake mzazi Hussen Saleh, ambaye alisema mwanae alikuwa kondakta wa daladala lingine hivyo alipata lifti tu kuwahi kwenda kufuata gari yake iliyokuwa eneo la Mbezi.
Wengine ni Faraj Ismail Ngalamba aliyekuwa kondakta wa daladala hilo, ambaye alitambuliwa na kaka yake baada ya kudai kuwa anampigia simu lakini hampati. Abudultwaibu Twalib, aliyetambuliwa na mke wake, Shani Mustafa ambaye alikuwa anawahi kazini bandarini, Easter Paulo mwanamke aliyekuwa mjamzito aliyetambuliwa na ndugu zake baada ya mwili huo kuvutwa huku tumbo kuchanika. Pamoja na maiti ya Zainabu Ali.
-Picha na habari na Yusufu Bandi wa TSN.



No comments:

WATEMBELEAJI