Monday, July 12, 2010

NIPO SAFARINI NAELEKEA NYUMBANI TANZANIA!

Nipo safarini naelekea nyumbani Tanzania kwa likizo kidogo na kushughulikia maswala mbalimbali ya kikazi na kunyonya kidogo kwa mama, maana mtoto hakui kwa mama, maana huwa wanasema naenda kunyonya kidogo kwa mama. Sasa basi nipatapo tu nafasi na mtandao mzuri, tutaendeleza kijiwe chetu kama kawaida, kama mnavyojua mtandao wa nyumbani ni wa kwi kwi kwi! Lakini nipo pamoja nanyi daima nami nitajitahidi. Nategemea kuwasili kesho usiku Jijini Dar, nimekukumbuka sana wewe mpendwa wangu wa moyo wangu Tanzania, nami nakuja sasa kukusalimu Tanzania wangu.

-Ninawasalimu sana nyinyi nyote wadau wangu, natupo pamoja daima!

1 comment:

mangi said...

"WELCOME TO TANZANIA THE LAND OF KILIMANJARO,ZANZIBAR,THE SERENGETI AND THE BUSINESS BRIDGE TO GREAT LAKES CONTRIES VIA DAR ES SALAAM PORT"
-----------------------------------
"Jasiri haachi asili na muacha asili ni hasidi na hana akili".
-----------------------------------
Ukifika Dar tafadhali sana nipigiiiiiiiie.!!!!

WATEMBELEAJI