Saturday, September 11, 2010

NAWASHUKURUNI SANA KWA SALA ZENU; NIMERUDI SALAMA!

Asanteni sana kwa sala zenu, nimewasili tena hapa Ugaibuni na safari zangu zote zimeenda vizuri sana, baada ya kumaliza likizo yangu salama huko nyumbani Tanzania. Ninamasikitiko sana kuiacha Tanzania yangu, lakini basi ndo maisha yanavyo kwenda, ipo siku tutakuwa pamoja Tanzania wangu endelea kunivumilia tu! Nitakuja tukae pamoja daima, sita kuacha daima milele Tanzania!

Asanteni sana wadau wangu, kwa kunivumilia mpaka nimerudi tutaendelea kuwa pamoja daima...na tutaendeleza libeneke tena. Na kwa wale waliopo Tanzania ambao hatukuweza kuonana, nawaomba msamaha sana ambao sikufanikiwa kuonana nao, kutokana na majukumu niliyokuwa nayo, nawaombeni mnisamehe, ipo siku tutaonana tu! Asanteni sana na WEEKEND NJEMA NA JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NYOTE!

-B.CHIBIRITI.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Baraka karibu sana tena hapa na nashukuru umekuwa na muda mzuri pia kila ulichofanya kimekuwa salama.

Baraka Chibiriti said...

Asante sana tena sana Dada Yasinta, tupo pamoja daima.

WATEMBELEAJI