Monday, October 4, 2010

TAARIFA YA MSIBA WA JAMAA NINAE MFAHAMU KWA UKARIBU!

Nimepata taarifa ya msiba wa jamaa ninae mfahamu sana, na alikuwa kijana mwema sana. Nikiwa likizo hivi karibuni mara nyingi nilikuwa nae hapo Tegeta, taarifa hii imenishitua sana tena sana na kuhuzunika sana, maana nilimwacha akiwa mzima kabisa. Taarifa inasema alienda kulala akiwa mzima kabisa asubuhi hakuamka tena, mke wake alimwamsha lakini mauti yalikuwa yamesha mkuta tayari. Ni kijana ambaye alikuwa anafahamika sana hapo Tegeta, kwa ucheshi wake, kwa kuimba kwaya katika kanisa kuu la RC Parokia ya Tegeta.
Kwakweli sisi hapa Duniani ni wapita njia tu!

Devi kama tulivyo zoea kukuita,,... sisi tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi. Hatuna jinsi..ki mwili hatupo nawe tena, lakini ki roho upo nasi daima na utabaki mioyoni mwetu daima.

David...Mungu ailaze Roho yako mahali pema peponi...Amina!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana kwa msiba. maana kufiwa na rafiki kama huyo ni pigo kubwa sana. Tupo pamoja.

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada Yasinta, kwakweli ni pigo kubwa sana kwangu.

WATEMBELEAJI