Wednesday, November 24, 2010

GARI HII INAITWA PANDA - NAMI HUWA NAIITA PUNDA!





Gari ndogo aina ya Panda - Fiat, ni gari ya Kiitaly ambayo ni maarufu sana hapa Italy.
Ni gari ndogo ambayo inauwezo mkubwa sana wa kuparamia milima na mabonde, pia kufanya kazi nzito kama uvutaji wa trela kama tuonavyo hapo kwenye picha. Mimi napenda sana magari madogo, maana huwa sioni umhimu wa kuwa na ligari kubwa mjini ambalo halina kazi yoyote, ilimladi uonekane kwa watu kuwa una gari la kifahari. Gari kama hizi hupunguza ghalama nyingi sana na kupaki mijini ni rahisi sana. Siku moja Tanzania nilisema hivi rafiki yangu mmoja alikasirika sana, kwani yeye ni mpenda magari makubwa kama mashangingi. Sikatai kuwa nalo, yanasaidia sana vijijini, kwa shuluba za huko. Lakini huwa naona hata hapa nilipo Cesena, watu wengi wana mashangingi, huwa najiuliza sana ya kazi gani mjini? pia wanahangaika kupaki na kuingia sehemu zingine. Wakati Panda - mimi huwa naiita Punda, kinabeba shehena ya kutosha katika trela lake na kuparamia milima kama hakina akili nzuri, na kinaenda sehemu yoyote ile. Nilijaribu kwenda milima ya Austria, na theruji ilikuwa ya kutosha watu wengi walishindwa kupanda mlima na mashangingi yao, lakini mimi nilipanda bila shida yoyote. Nilipo weka 4x4 na muziki kwa mbali, waliniona kwa mbali ninavyo waacha kwenye theruji, wenyewe na shangingi yao wamebaki midomo wazi. Panda aka Punda....we acha tu, usikaone kadogo hako kana mambo makubwa!

No comments:

WATEMBELEAJI