Monday, December 6, 2010

HA HA HA HAAAAA.......HUU UBECHE LEO LAZIMA ULIWE TU!







Mkuu Beda....wa LUKWANGULE, akiwa likizo kijijini kwao huko Morogoro kwa raha zake, mpaka namwonea wivu kwa mambo mazuri kama haya ya kijijini. Hakuna kitu nilichokuwa napenda kama kutwanga mpunga enzi zile huko Kijijini kwetu, nikiambiwa nitwange mambo mengine ni ugomvi tu,ila mpunga huniambii kitu. Maana ilikuwa ni furaha sana kwasababu nilijua tu kuwa lazima nile ubeche, mchele aka wali..ubwabwa! Nilivyokuwa naupenda hata kama nilikuwa nimechoka nikiambiwa jioni tunakula ubwabwa, niliulizwa; unaweza kutwanga? We nguvu zilikuwa zinarudi haraka sana...mbele ya ubwabwa? We acha tu!


No comments:

WATEMBELEAJI