Sunday, November 13, 2011

TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI HII NJEMA!

Yesu mpendwa wangu, njoo moyoni mwangu karibu nakukaribisha, naumia moyoni mwangu...njaa, kiu vinanitesa....kimbilio langu ni wewe tu! nimekuja unilishe mwili wako na uninyweshe damu yako nipate uzima wa milele!
Najongea meza yako...wewe wanikaribisha, Yesu wewe ni mwema sana kwangu, Yesu wewe ndiwe faraja yangu. Yesu wangu nguvu yangu, wewe ndiwe tegemeo la maisha yangu yote. Wewe ndiwe kitulizo cha roho yangu milele! Bila wewe sina nguvu kabisa kukabiliana na mambo magumu katika haya maisha, roho yangu ni dhaifu...mwili wako ni chakula cha kunipa nguvu, na damu yako ni kinywaji changu......nilishe na uninyweshe siku zote za maisha yangu.

No comments:

WATEMBELEAJI