Dondokeni enyi mbingu, toka juu.... na mawingu na yammwage mwenye haki; nchi ifunuke na kumtoa Mwokozi.
Tunaomba ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu...ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba; Kristu Mwanao amejifanya Mtu....kwa mateso na msalaba wake, tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko.
Ee Mungu Mwenyezi, tumekwisha pokea amana ya ukombozi wa milele. Tunaomba jinsi tunavyoikaribia hiyo sikukuu takatifu.....hivyo tuzidishe Ibada yetu, tupate kuliadhimisha vema fumbo la kuzaliwa kwake Mwanao.
No comments:
Post a Comment