Wednesday, May 12, 2010

HIVI WEWE NI MKAMILIFU MPAKA UMHUKUMU MWENZIO HIVI??

Wakati mwingine binadamu tunakuwa na ukatili sana kushinda hata wanyama wakari. Mimi huwa najiuliza sana kwanini tunakuwa wakatili kiasi hiki cha kuhukumu kifo wenzetu...kwani sisi makosa yetu hayastahili kuhukumiwa kifo kama tufanyavyo kwa wengine?? Je sisi ni wakamilifu sana kiasi cha kuhukumu wengine? Mbona hata sisi makosa yetu yanastahili kuhukumiwa...vipi sasa? Mungu peke yake ndiye anayetoa hukumu ya kifo kwa watu kwanini ujichukulie uamzi huu mzito hivi. Najua sana si kitu rahisi sana kusamehe hasa kwa makosa mengine makubwa ambayo sitaki hata kuyataja, lakini si kufikia uamzi huu...sisi sote ni binadamu tu na kila mtu anamapungufu yake, ipo siku na wewe utakuja kukosea hivi, sikutakii hivi bali nakutakia mema mengi sana, lakini kumbuka na wewe ukikosea hivi...ufanyiwe hivi??? Je utakubali na kuridhika na kusema wanahaki wanao nihukumu kwa kosa hili nililo fanya?????

No comments:

WATEMBELEAJI