Tuesday, May 11, 2010

ULONGONI - GONGO LA MBOTO - DAR ES SALAAM.




Nadhani kama si kitu kuwa ofisi muhimu za kiserikali na shughuli za kijamii zipo kwa wingi Jijini Dar es salaam, sidhani kama kungekuwepo na watu wanaopenda kuishi katika hali hii ya msongamano. Ni utitiri wa vitu na watu walioamua kuapa ''kubanana hapa hapa hadi kieleweke''...ingawaje kwa hali halisi ya walio wengi, haifahamiki wala kujulikana kitaeleweka lini. Matokeo yake ni msongamano kila kona, nyumbani msongamano, barabarani msongamano, shuleni msongamano, ofisini msongamano, nyumba za ibada msongamano, mahakamani msongamano, hospitalini msongamano, kumbi za starehe msongamano, nyumba za wageni msongamano na makaburini msongamano......keero kero!
Ama kweli hili ni Jiji la Bongo msongamano!
-WAVUTI.


No comments:

WATEMBELEAJI