Tuesday, June 8, 2010

SASA CHAI TUTAWEKA WAPI?

Nimekutana nayo hii kwa Wavuti, nimecheka sana...!!!! Kombe la Dunia ninapigiwa plani ili litumike kwa chai? Lakini ingelikuwa sio mbaya sana mawazo haya...maana kwa bei linavyo uzwa watu wengi duniani, jinsi wahangaikavyo...wangeweza kula na kunywa kwa hela hizo za kombe hili. Si kutumia kunywea chai tu bali kuwashibisha hata watu wengi wenye njaa. Wakati mwingine huwa najiuliza sana, haya mambo ya mashindano kama haya yanasaidia nini...kutumika kwa ghalama zote hizi wakati watu duniani wanakufa na njaa? Mimi ni mpenzi sana wa mpira...wakati mwingine huwa nasikitika sana tena sana, hela zinavyotumika kwa mpira tu! wakati watoto taifa la kesho wanakufa kwa kitu kidogo sana kwa kukosa pesa za matibabu...hivi kweli mbele za Mungu tutajibu nini kuhusu mambo haya???? Kazi kweli kweli....!!!!!

-Credit; Mtwara kumekucha blog/Baraka Mfunguo.



1 comment:

mangi said...

NDUGU YANGU BARAKA UMESEMA KWELI NA UMEUGUSA SANA MOYO WANGU KUHUSU UDHAIFU WA BINADAMU KUZIDI KUHANGAIKIA MAMBO MAKUBWA YA BURUDANI TU NA KUSAHAU VIPAUMBELE MUHIMU MAISHANI MWAKE.JANA KWENYE TAARIFA YA HABARI YA TBC1 HUKO MUHEZA KATIKA SHULE YA MSINGI YENYE WANAFUNZI 250 NI MMOJA TU ANAVAA VIATU,WAWILI WANAVAA YEBOYEBO,247 WANAPEKUA NA MAZINGIRA DUNI YA KUSOMEA BILA MADAWATI.KWA UJUMLA MIUNDOMBINU DUNI KATIKA SEKTA ZA ELIMU,AFYA NA USAFIRISHAJI BARANI AFRIKA NI TATIZO ENDELEVU.

WATEMBELEAJI