Vifo vingi hutokea kwa kukosa misaada na kutomudu ghalama za matibabu, yatupasa tusaidiane. Uonapo ndugu, jamaa na marafiki wagonjwa nawe una uwezo wa kuwasaidia....saidia! Uonapo barabarani ajali imetokea na watu kujeruhiwa, wanahitaji msaada wako wa hali na mali...saidia! Tuwasaidie vema ili kutokupoteza maisha yao ki ulaisi laisi tu! Mara nyingi ajali zitokeapo watu hukimbilia mali kwanza, kwa kuiba kila kitu. Huacha watu wakiteseka kwa kubanwa kwenye vyuma vya gari, kwanini usisaidie kwanza binadamu mwenzio ndipo uibe hivyo vitu unavyotaka?
Jamani tuwe na moyo wa huruma tuonapo ajali kwa majeruhi wetu na kwa wagonjwa wetu kwa ujumla majumbani mwetu tuwahurumie kwa kuwasaidia. Kwani hatujui ipo siku hata sisi tutahitaji msaada huo huo, .... tubadilike na tujenge tabia ya kupenda kuwajali wengine, yatupasa tusaidiane ki ukweli.
Pia siku hizi maradhi mengi yameibuka, ambayo husababisha vifo vingi na wagonjwa wetu kuteseka, basi tuwaonee huruma sana wagonjwa wetu.
Ingawa kuishi ni bahati tu! na kufa ni lazima tu! kwetu sote, hivi ni vizuri wanandugu, wanajamii kupanga mikakati kuchangia kuokoa maisha yao wagonjwa wetu, ili kuokoa vifo visivyo vya msingi katika jamii yetu, ili visitokee mara kwa mara bila sababu.
Nani kauona mwaka, kamaliza mwaka....ni majaliwa yake tu! Mwenyezi Mungu.
Ni vizuri ndugu, jamaa na marafiki kuweka vikao na kujadili ghalama za matibabu, kuliko kuwatelekeza wagonjwa hawa bila msaada wowote, inapaswa kutetea maisha yao wanapokuwa wanaumwa. Mbona vikao vya harusi tunaweza sana kuchangia kwa hali na mali, sasa wagonjwa kwanini tusiweze pia? Wagonjwa hawa wakishakufa badala yake tunaonesha ufahari misibani, wa kuchangia huku na kule, kwanini tusichangie wanapokuwa wagonjwa?
Tabia hii ki binadamu haifai kabisa, jamani tuwe na huruma kwa wagonjwa wetu....kuugua sio kufa!
- SAIDIA WAGONJWA, NAWE IPO SIKU UTAKUJA KUHITAJI MSAADA HUO HUO....NAWE UTAKUJA KUSAIDIWA!
- Baraka.
No comments:
Post a Comment