Sunday, March 6, 2011

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII....

POKEA SIFA NA UTUKUFU EE MUNGU BABA YETU!


Pokea sifa na utukufu kwa mengi uliyo tutendea, tungependa kuyataja yote...lakini hatuwezi.
Milima na mabonde umetuvusha, mabaya na mazuri tumepokea, tunasema asante sana kwa wema wako.

Umefanya kwa wingi sana Baba, wala hatuwezi kuyahesabu, tukufananishe na nini Baba yetu...hakuna cha kukufananisha nawe Mungu Baba Mwenyezi. Tuseme nini juu ya mambo yako makuu uliyo tutendea?

Tuseme nini juu ya mambo hayo makuu, Mungu ukiwa upande wetu, je ni nani atakaye tutenga nao upendo wako? Hakuna! Tutashinda zaidi ya kushinda kwa nguvu zako wewe Baba yetu...ututiae nguvu siku zote!

No comments:

WATEMBELEAJI