Wednesday, February 29, 2012

MZEE WA KIDUKU; MARLAW......NA MBAYUWAYU!



Mimi binafsi huwa namwita Marlaw (Mzee wa Kiduku) maana mwendo wake wa kucheza ni wa kiduku kiduku vile!

NAFAKA ZAPAISHA KATA ZA CHAKWALE NA RUBEHO!

WAFANYABIASHARA WAKIUZA MAHINDI KATIKA SOKO LA KIBAIGWA.


Tarafa ya Gairo katika Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro.......imepata mafanikio makubwa sana hasa katika Sekta ya Kilimo, kutokana na Wananchi wake kuwa wazalishaji wakubwa wa Mahindi, Viazi vitamu, Alizeti na Ufuta. Pamoja na kilimo cha usalishaji wa mazao hayo, pia sehemu kubwa ya Wananchi wake ni wafugaji wa mifugo ya aina mbalimbali hasa ng'ombe na mbuzi.
Kutokana na mafanikio katika nyanja hiyo, Wananchi wa Tarafa hiyo hasa kutoka Kata ya Chakwale na Vijiji vya jirani pamoja na Kata ya Rubeho, wamekuwa na hamu kubwa sana ya kuendeleza mafanikio hayo kupitia Nishati ya Umeme.......lakini mpaka sasa umeme bado haujafika! Wahusika mpo hapo?....mnasikia kilio hiki?

- Habari na Mkuu John Nditi.

GARI LA POLISI LIKIWA CHOBINGO........USALAMA KWANZA!

Askari wa Usalama Barabarani eneo la Inyala, Mkoani Mbeya......wakisimamisha magari kuangalia usalama, leo asubuhi.

- Picha na Mkuu Lukwangule.

UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA UNAOFANYWA NA KIWANDA CHA SARUJI CHA WAZO HILL - JIJINI DAR ES SALAAM!.


Habari za leo.....kwa masikitiko makubwa sana sisi Wananchi tunaoishi maeneo ya karibu au pembezoni mwa Kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill, Jijini Dar es salaam....tunaathirika na uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na moshi na vumbi wa Kiwanda hicho!
Kama unavyoona katika picha zote mbili......tunaomba kufahamishwa kama kuna hatua zozote zinazochukuliwa au kudhibitiwa na mamlaka husika NEMC.....jamani je tutapona kweli kwa hali kama hii???

- Mdau Mwanamazingira.

NIMEKUCHAGUWA WEWE...UWE WANGU WA MAISHA!

HAPA NI UBUNIFU WA HALI YA JUU WA KUKATA UKOKA!

UBUNIFU WA KUKATA MAJANI a.k.a UKOKA. SAYANSI NA TEKELINALO KUIJIA.

MAMBO YA KUZIBA PANCHA....ILULA - IRINGA. 2011.


Tulipata pancha, tukitokea Makalala - Mafinga - Iringa....sehemu ya Ilula, baadae tulipata sehemu ya kuziba tairi kabla ya kuendelea na safari yetu ya kurudi Dar es salaam. Nilipata pia nafasi ya kuongea (kupiga story kidogo) na hawa vijana wa Kijiwe hiki cha kuziba pancha cha Ilula, wanachekesha sana tena sana....nilicheka mno, na kusahau kabisa shida na matatizo niliyonayo, mara nyingi huwa tunajisahau sana ukipata shida kidogo tu, unalalamika weeee...!!! hujui kumbe kuna wenye shida zaidi yako. Vijana hawa pamoja na kuwa na uchumi wao mdogo, lakini hapa ni full shangwe haswa. Nilijiona kwakweli mimi ni mlalamikaji tu, hakuna cha shida wala tabu. Walinichekesha mpaka leo nakumbuka kwa hili, Walisema; Hapa huwa wanakuja wenyewe Viongozi wakubwa na vitambi vyao kuomba tuwazibie pacha, huwa wakati mwingine wanakuja kwa kuamrisha ziba haraka nina safari ndefu, na sisi tukiona hivyo ndo kwanza tunalegeza uzi, utaona wenyewe wanaanza kuomba kwa utaratibu - wananywea wenyewe! Kazi ya mtu ni kazi tu...lazima uiheshimu bwana, kwani mimi sio binadamu kama yeye? hata awe nani akifika hapa lazima atulize mpira tu! Sisi hatumwibii mtu, tunafanyakazi na kujali watu wanaotujali...ukileta ubishi wako na sisi tunakuwa hivyo hivyo, walisema vijana hawa.

Nilicheka sana na kufurahi mno kwa msimamo wa hawa vijana....kweli inatakiwa iwe hivi; heshimu kazi ya mwenzio, hata uwe mkubwa kiasi gani...heshimu wadogo tafadhali.

Tuesday, February 28, 2012

KAWE DARAJANI....LEO ASUBUHI WAMEBANDUANA!


Mambo ya Jiji la Dar es salaam....a.k.a Bongo, kila siku lazima yatokee kama haya, hata uwe mwangalifu kupita kiasi....lakini wapo vichaa kama hawa wa Daladala lazima tu wakubandue!

- Picha na Mzee wa Jiachie, Michuzi Jr.

HAPA JE?......HATARI LAKINI SALAMA!

JE INGEKUWA HIVI..... INGEKUWAJE?

KIDOGO LAKINI GUSA BEI YAKE UONE CHA MOTO!

Hivi vigari vina bei mpaka unashangaa, na watu wanavipenda sana....bei yake unaweza ukanunua Gari za kawaida kama tatu au nne kabisa.

Monday, February 27, 2012

VIDEO MPYA YA BIBI CHEKA ft.MH.TEMBA - NI WEWE!

MAJUKUMU YA ULEZI KWA KARNE HII NI YA WOTE!

Majukumu ya malezi ya watoto kwa karne hii ni ya wote......haijalishi jinsia, pichani Bwn.Gibson Mwalibwa, akiwa amembeba mtoto wake wa mwaka mmoja na miezi 8, wakati Mama mzazi akipata huduma za matibabu kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

- Blog hii inakupa hongera sana bwana Gibson, kwa kuonyesha mfano mzuri kwa akina Baba wote....na kuwaambia ujumbe huu mzuri; Kulea watoto ni jumkumu la wazazi wote wawili, sio kazi za akina mama peke yao tu....hata akina baba pia ni jukumu letu sote.

- Picha na Michuzi Jr.....a.k.a Mzee wa Blog ya Jiachie.

NOEMI........SONO SOLO PAROLE!

POLISI WAMUOKOA PADRI KANISANI..........

Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Lugoba, Jimbo la Morogoro, Padri Philipo Mkunde.....amezuiwa na waumini kuongoza Misa Takatifu baada ya kudaiwa kuwakashifu Waumini wa Kabila la Wakwere. Padri Mkude, alizuiwa kuongoza misa ya hapo jana Jumapili asubuhi Parokiani hapo baada ya Waumini zaidi ya 200 kuandamana wakiwa na mabango zaidi ya 20 wakidai ahamishwe kwa kuwa amewatukana katika mahubiri yake, kwamba; watoto wao ni wachafu na wao wamebakia kucheza ngoma badala ya kufanya maendeleo.

''Tumechoka na mahubiri ya huyu Padri, kila akihubiri Kanisani lazima atuseme Wakwere, tumekosa nini??'' Mara atuseme tu maskini, mara watoto wetu ni wachafu na hatuwapeleki shule tunashindia ngoma tu....tumechoka hatumtaki kabisa (walisema Waumini maneno haya)''.

''Leo tumemzuia asisome misa kabisa, hakuna haja maana hakuna amani Kanisani hatujui ana kitu gani na sisi, sijui kwasababu Parokia hii ni Wakwere?''
Hata Jumatano ya Majivu wiki iliyopita katusema sana, eti watoto wetu ni wachafu sana ukilinganisha na Makabila mengine Tanzania, hii ni kashfa sana kwetu sisi, walisema hivi Waumini hawa wa Parokia ya Lugoba.

Wakwere ni moja ya Makabila katika Mkoa wa Pwani, linalopatikana Wilayani Bagamoyo....lakini katika mfumo wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Lugoba ipo chini ya Jimbo Katoliki la Morogoro.
Hali hiyo imesababisha watu wengi kutokwenda Kanisani wakijua leo Padri huyo anaongoza Misa, lakini akiongoza Katekista....Ibada inajaa utadhani Askofu amekuja, tunachotaka hapa ni Padri mwingine, kama Askofu anatujali atuletee Padri mwingine ''(walisema hivi Waumini hao)''.

- Habari na Gloria Tesha.

HAWA NI WAZEE WA KAZI NA TRIPU KWELI...WAZEE WA OVERLAND!





JIJI LA DAR ES SALAAM....LINAZIDI KUPENDEZA TU!

MOSHI OUR HOME!......WACHAGA MPO HAPA?

Kirefu cha mji wa Moshi ni huu hapa.....MUNGU ONYESHA SEHEMU HELA ILIPO.

Sunday, February 26, 2012

TUZO YA HESHIMA KWA MAMA MARIA NYERERE!

KARANGA KWA WINGI DODOMA......KARIBUNI SANA!

Rafiki Peter Fumbi, akitukaribisha Dodoma.....anasema karanga kwa wingi Dom!

- Picha na Peter Fumbi.

MITAA YA BUKOBA........TANZANIA!



- Picha na Mdau wa Bukoba Blog.

MILAN - JUVE. 1-1..NA SHABIKI WA MILAN, TIZIANO CRUDELI.

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA DODOMA!

Mwenyekiti wa UVCCM - Mkoa wa Dodoma, Ndg.Anthony Mavunde, akiwasili katika viwanja vya shule ya Sekondari Sejeli - Kongwa, Dodoma......katika ziara ya siku moja iliyoambatana na ufunguzi wa Tawi la UVCCM Sekondari ya Sejeli ambapo vijana zaidi ya 200 walijiunga na UVCCM....tarehe 25.02.2012.

- Picha na Anthony Mavunde.

JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU!

MANENO MAZURI YA JUMAPILI YA 1 YA KWARESIMA!

Ataniita nami nitamwitikia....nitamwokoa na kumtukuza, kwa siku nyingi nitamshibisha.

Ee Mungu Mwenyezi, utujalie tuzidi kuifahamu siri ya Kristu na kupata manufaa yake katika mwenendo wetu mwema kwa mfungo wa Kwaresima wa kila Mwaka.

MTU HATAISHI KWA MKATE TU, ILA KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU.

BWANA ATAKUFUNIKA KWA MANYOYA YAKE, CHINI YA MBAWA ZAKE UTAPATA KIMBILIO.

Friday, February 24, 2012

MIKESE - MOROGORO....KWENYE MATUNDA!

CHALINZE.

SAFARI YA DAR ES SALAAM TO SINGIDA -VIJIJINI. 2011.

Picha ya pamoja na Dereva a.k.a Suka Vicent...tukiwa Chalinze.
Picha ya pamoja na msaidizi wa Dereva, Maiko.


MWANZA CITY - TANZANIA.


Nalipenda sana Jiji la Mwanza, kwa mawe yake mazuri....mimi na mawe ni marafiki sana!

OOOOOPS........MZEE UMEUMBUKA!

Thursday, February 23, 2012

TAYARI SAFARI INAANZA...HAPA TUKITOKA UBUNGO-DAR.



DEREVA VICENT...AKIONYESHA VITU VYAKE HAPA.

SAFARI ILIANZA NA LORI...KUPELEKA DAWA HOSPITAL.2011.

Tunajiandaa kwa safari ya kwenda huko Sindida Vijijini, tukitokea Dar es salaam, kupeleka dawa Hospitalini...na mimi sikukosa kuwepo. Hii ilikuwa katika likizo yangu ya Mwezi wa 8 Mwaka jana.
Mafuta a.k.a (Wese) likiwekwa tayari kuanza safari ya KM 500..kwenda Singida.
Dereva...ngoja ninunue zawadi ya matunda na mboga kwa watoto. Hapa maeneo ya Mikese - Morogoro.
Minzani ya Kibaha, katika kupima uzito.
Chalinze...kunywa chai kidogo.

HAPA JE?......HATARI LAKINI SALAMA!

Wednesday, February 22, 2012

KWARESIMA NJEMA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU!

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Eusebius Nzigirwa......akipaka majivu Waamini leo.... kama ishara ya kuanza mfungo wa Kwaresima.

- Nami nasema; Tubuni na kuiamini Injili.

NDOA NDOANA......KUTOKA KWA ORIJINO KOMEDI - TANZANIA.

CHAGUA MWENYEWE HAPA........

MAMBO YA JESHI NI BALAA TUPU......

Utakula tu...labda uwe hauna njaa, mayai yanapikiwa kwenye koleo. Jeshi sio lelemama!

Tuesday, February 21, 2012

MALEO WANGU.....MAMBO YA DODOMA HAYA! a.k.a DOM.



Mambo ya Dodoma a.k.a DOM au ukipenda Idodomya....mtafute Mgogo harisi akutafsirie hapa, mimi kigogo changu sio kizuri sana, lakini maneno machache nitajitahidi kutafsiri;


- Maleo nitafanya nini mwenzako......swala hilo Maleo linaniumiza sana.....nikiwa nimekaa mbugani nawaza sana mwenzako.......nitaongea na nani mimi?..........

MTOTO WA WHITNEY HOUSTON...AKUTWA AKIBWIA UNGA.

NEW JERSEY, MAREKANI; Mtoto wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown.....anadaiwa kufumwa akivuta madawa ya kulevya masaa machache tu baada ya mazishi ya mama yake.

Inadaiwa masaa manne hivi baada ya shughuli za mazishi kumalizika, Bobbi Kristina (18) akiwa na rafiki zake pamoja na ndugu.....ghafla alitoweka na kwenda kusikojulikana. Ingawa mtu wa karibu na familia ya Houston alisema; Kristina....alipelekwa kwenye kituo cha mafunzo ya kuacha dawa za kulevya mwaka jana.
Binti huyu mzuri, amekuwa huku akimuona Mama yake akitumia dawa za kulevya. Familia yake imekuwa na wasiwasi mkubwa wa Kristina kufuata nyayo za Mama yake.

90-YR-OLD GRANDMA DANCES TO WHITNEY HOUSTON'S.



90-Yr-Old GrandMA dances to Whitney Houston's - I Wanna dance with somebody.

- Maisha ni kufurahi bwana....ndo maana Bibi kaishi miaka mingi, sio mchezo! Furaha ni muhimu sana katika maisha haya, mimi ningeweza.....ningeweza kufurahi daima siku zote!

JIJI LA DAR ES SALAAM LIKIZIDI KUPENDEZA KILA KUKICHA!

BURUDIKA NA KIBAO HIKI MOTOMOTO!

HUWA NASIKITIKA SANA...UMASKINI WETU HUU JAMANI.

Mtoto kama huyu anatakiwa awaze masomo tu, hakuna kingine....

HAYA SASA....UKISIKIA FUMANIZI NDO HII.

Monday, February 20, 2012

NAPE......NAYE KATIKA MAOMBI YA DHAMBI YA MAFISADI.

HATARI HII...PIKIPIKI MOJA WATU 5 (WAKIWEMO WATOTO WADOGO).

Mwendesha Pikipiki katika Manispaa ya Morogoro, alimaarufu kama Bodaboda....akiwa amewapakia abiria wanne, jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria za Usalama Barabarani, wakati akiwasafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine....ambapo ni hatari sana kwa usalama wa maisha yao.... kama alivyonaswa na Kamera ya Juma Mtanda, katika eneo la Kihonda, Kanisani - Katika Mji kasoro Bahari.

- Picha na Subi (kwa hisani ya Juma Mtanda).

TAARIFA YA HABARI KWA HISANI YA.........ITV!

GHOROFA LA KISASA.......DODOMA - TANZANIA.


- Picha kutoka kwa rafiki; Peter Fumbi
Dodoma - Tanzania.

MISELE YA HAPA NA PALE......IMEANZA TENA KAMA KAWAIDA!

NJIA YA KUINGIA MASKANI........


Hatimaye ndoto mbaya imekwisha sasa.......

WATEMBELEAJI